Protein Powder
Viungo:
Soy Protein Isolate, Peanut Protein Powder, Soybean Lecithin
Kazi Na Faida Zake
- Husaidia ukuaji wa mwili wa binadamu
- Hufanya shughuli zilizoainishwa na genes
- Hutunza vimeng'enya ambavyo huchochea mabadiliko ya kikemikali
- Huhusika katika utoaji taarifa wa seli na usafirishaji wa viambata vya genes kutoka seli moja hadi nyingine
- Umbo la protini huleta ugumu katika maumbile laini ya viungo vya kibaolojia
Yafaa Kutumiwa Na:
- Watu walio na utapiamlo kama wanaotumia vilevi
- Watu walio katika hali mbaya za magonjwa kama wenye saratani, UKIMWI, TB, kisukari, n.k.
- Watu wasio kula nyama, wenye upungufu wa protini
- Wanariadha wanaohitaji kujenga misuli
- Watu walio kwenye mpango wa kudhibiti uzito/unene wa miili yao
Maelezo Muhimu:
Umuhimu Wa Protini
Protini ni moja ya virutubishi muhimu katika maisha yetu. Shughuli zote za mwili; uvunjajivunjaji na ujenzi wa kemikali katika mwili (umetaboli), ujenzi wa mifupa, uundaji wa viungo, ukarabati wa tishu za mwili na utoaji wa nishati, haziwezi kuendelea bila ushirikishwaji wa protini. Ukuaji wa mwili, ukarabati wa tishu zilizoumia, uvunjaji na ujenzi wa kemikali, utengenezaji wa vimeng'enya, kinga za mwili, ulinzi wa uhai, kuahirisha uzee na maisha marefu, vyote havifanikiwi bila protini.
Ukosefu Wa Protini
Kutokupata kiwango kinachofaa cha protini kutasababisha viungo vingi vya mwili kutofanya kazi vizuri, kumbukumbu kupungua na kusinyaa kwa viungo vingine, ngozi kulegea, udhaifu wa misuli, na magonjwa mengine mengi.
Kiasi Gani Cha Protini Tunahitaji?
Mahitaji yetu ya protini yatategemea umri, maumbile ya mwili, na shughuli tunazozifanya. Kanuni ya kawaida inayotumiwa na wataalamu wa lishe wengi katika kukadiria mahitaji ya protini ya mwili kwa siku ni kuzidisha uzito wa mwili katika kilo kwa 0.8, au uzito wa mwili katika pounds kwa 0.37. Hizi ndizo gramu za protini ambazo mwili lazima upate kila siku. Kwa njia hii, mtu mwenye kilo 60 anatakiwa ale gramu 48 kwa siku.
Tahadhali:
Watu wenye matatizo makubwa ya ini na figo lazima wadhibiti matumizi ya protini. Kwa hiyo bidhaa hii haifai kwa wale wenye maini au figo ambazo hazifanyi kazi vizuri.
<<<<< MWANZO